Bwalya
UONGOZI wa Simba umefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wao mshambuliaji raia wa Zambia Rally Bwalya kwa timu ambayo hawajaiweka wazi kutokana na matakwa ya kimkataba.

Taarifa rasmi iliyowekwa kwenye Simba App, imeeleza kuwa, Bwallya atacheza mchezo wake wa mwisho Jumapili hii dhidi ya KMC na baada ya hapo ataruhusiwa kuondoka kwenda kujiunga na timu yake mpya kuanza maandalizi ya msimu (Pre Season).
Bwalya alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja

Taarifa hiyo imeeleza, kwa heshima ya mchezaji ambaye amedumu na Wekundu hao wa Msimbazi kwa misimu miwili, watautumia mchezo huo dhidi ya KMC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar, kumuaga rasmi nyota huyo wa Zambia.

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 kutoka Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo mpaka anaondoka kwenda timu mpya alikuwa amebakisha kandarasi ya mwaka mmoja.